3 Julai 2025 - 11:53
Source: ABNA
Mlipuko Pakistan Waacha Wanne Wakiwa Wamekufa na 11 Kujeruhiwa

Mlipuko wa bomu kaskazini-magharibi mwa Pakistan umesababisha vifo vya watu wanne na kujeruhiwa 11.

Kulingana na Shirika la Habari la AhlulBayt (ABNA), mlipuko umetokea katika eneo la Bajaur, lililoko katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, Pakistan.

Afisa mkuu wa serikali pia ni miongoni mwa wahanga wanne wa mlipuko huo wa bomu na magari kadhaa ya serikali pia yameharibiwa katika tukio hilo.

Polisi imesema kuwa angalau watu 11 walijeruhiwa katika tukio hilo na hali ya baadhi yao ni mbaya na idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Hadi sasa, hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na mlipuko huo kaskazini-magharibi mwa Pakistan.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha